Mtoto wa mwimbaji wa R&B Usher Raymond aitwaye Usher Raymond V aliyepata ajali ya maji wiki iliyopita amepona na kuruhusiwa kutoka hospitali.
![]() |
Usher Raymond na Mtoto wake |

Jana kamera za TMZ zilimuotea Usher Raymond V mwenye miaka 5 akiwa na bibi yake wakitoka katika moja ya sehemu za michezo ya watoto iitwayo Mighty Jumps iliyoko Atlanta, Marekani huku akiwa amefungwa bandage katika mkono wake wa kulia.

Wiki moja iliyopita Usher Raymond V alinusurika kuzama katika bwawa la kuogelea lililoko nyumbani kwa baba yake lakini aliokolewa na kulazwa hospitali kwa siku kadhaa.