Kanye West awaagizia mwanae North na mchumba wake Kim Kardashian magari ya kijeshi




Katika kuhakikisha kuwa mwanae North na mchumba wake Kim Kardashian wanakuwa salama, Kanye West amewaagizia magari maalum yenye mfumo wa gari za kijeshi na ambayo hayapitishi risasi.


Kanye ameagiza gari aina ya Chevrolet Kodiak kwa gharama ya paundi milioni 250,000 ikiwa na muonekano wa “Limo One” gari ambayo Rais wa Marekani, Barack Obama hupanda.



Kwa Kim, Kanye ananunua gari yenye thamani ya paundi 800,000 aina ya SUV iitwayo Prombron Iron Diamond na iliyotengenezwa kijeshi na kampuni ya Latvia, Dartz Motorz Company.


Prombron Iron Diamond

Iron Diamond ilitengenezwa kuhimili risasi na mabomu ya kurushwa.
Previous Post Next Post

Popular Items