Mtandao wa San Jose Mercury News wa Marekani umeripoti kuwa mtanzania aitwaye Joseph Mackubi aliyekamatwa na kukutwa na hatia ya kutaka kuingiza dawa za kulevya aina ya Heroin nchini Marekani amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela Jumatano iliyopita (August 14).
Wakaguzi wa uwanja wa ndege wa Los Angeles (LAX) waligundua Lop top ya Mackubi ilikuwa na uzito usio wa kawaida baada ya kupitishwa katika mashine za ukaguzi (October) mwaka jana, hivyo wakaamua kuiwasha lakini ilikataa kuwaka. Kitendo cha laptop hiyo kugoma kuwaka kiliwashtua na kuhisi iko na kitu ndipo walipoamua kuifungua na kukuta ndani zimefichwa gram 800 ya dawa za kulevya aina ya Heroin.
Mackubi (33) aliyesafiri kwenda Marekani akitokea Nairobi alidai alikuwa anaenda Alabama kuonana na mwanamke waliyefahamiana katika Internet.
Mtandao huo umeongeza kuwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya aina hiyo yanayohusisha watanzania kukamatwa wakijaribu kuingiza dawa za kulevya katika uwanja huo wa ndege wa LAX nchini Marekani.
Mackubi anategemea kuanza kutumikia kifungo cha miaka 40 jela (September 11 ) mwaka huu nchini humo.
Source: San Jose Mercury News Picha: mtandaoni