Zikiwa zimesalia siku 15 msimu wa nane wa Big Brother kufikia tamati, mwakilishi wa Ghana Elikem ndiye mshiriki pekee aliyepata tiketi ya kuingia fainali za kinyang’anyiro cha $300,000 zawadi ya ‘The Chase’ mpaka sasa.
Elikem amefanikiwa kupata tiketi ya fainali jana (August 9) baada ya Big Brother kumtaja kuwa mkuu wa nyumba (HOH) wiki ya kuanzia Jumatatu (August 12). Kwa cheo hicho inamaanisha kuwa kutokana na kwamba wiki hii Elikem hayuko katika dangerzone tayari anauhakika wa kuwepo mchezoni wiki ijayo, na nafasi ya ukuu wa nyumba itamuwezesha kuivuka wiki ijayo salama na moja kwa moja itakuwa imebaki wiki moja tu ya fainali hivyo yeye hawezi kutoka tena mpaka fainali.
Mvua ya pongezi ilianza kumnyeshea Elikem kutoka kwa housemates mara baada ya Big Brother kutoa tangazo hilo na kumfanya atoe tabasamu kubwa.
Watazamaji wengi pia akiwemo aliyekuwa mpenzi wake Pokello waliipokea taarifa hiyo kwa furaha bila kujali utaifa wao na kusema Elikem anastahili nafasi aliyoipata.
-Pokello:My heart never lied to me. HOH all the way to the final! I believed in u then and I believe in u now, Ghana stand my and be counted!!! Elikem runs the city!
-Blessing Dafe: I am happy for Elikem; he won the head of house at the most crucial time. I am a Nigerian, but I hope that he wins BBA 2013. He deserves it more than any of the other housemates. He is kind and quite entertaining. Despite the fact that his fellow housemates constantly persecute him, for no justifiable reason, he still shows them love.
-Popo Maleka: I am a south African, I voted him over sulu coz he is emmotionally matured, to him winning the finale would be cherry on top, he mentioned it several times. He never talked about himself being in the top 5 , he was prepared for whatever outcome.He is humble and respectful, I like him for that. But I didnt like his triangle with Fatima and Pokello though.
-Matilda Anebelundu:am a nigerian but dis dude has rily shown how to fight for wot u want irrespective of any obstacle encountered on the way. Wot can i say but kudos to him… He deserves the moni though
Kitu kizuri ni kwamba Elikem ambaye wiki hii alipigiwa kura ya kuingia dangerzone hajui kama HOH alimuokoa na kumuweka Dillish, hivyo bado ana homa ya kutoka Jumapili hivyo itabaki kuwa suprise kwake mpaka kesho wakati wa eviction.