Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Barcelona sporting Andoni Zubizarreta amesema kwamba Manchester United imeachana na mpango wa kumsaini Cesc Fabregas.
United walituma ofa mbili zilizokataliwa na Barcelona kwa ajili ya kumsaini kiungo huyo mwenye miaka 26 na Barca wamekuwa wakirudia mara kwa mara kwamba hazuwi.
Huku kukiwa na tetesi kwamba United wanajiandaa kutuma ofa ya tatu, Zubizarreta ameliambia gazeti la Marca kwamba United wameachana na mpango wa kumsajili Cesc.
"Manchester United wameonyesha kuvutiwa na mchezaji, lakini pia wameshaelewa kwamba hatutaki kumuuza.
"Wameshaondoa suala hilo mezani. Hatumuuzi Cesc Fabregas."
Tags:
Sports