Oprah Winfrey kuja Tanzania wiki hii kwa ziara binafsi, atatembelea Serengeti




Malkia wa Talk Shows na mwanamke wa pili mweusi kwa utajiri duniani (nyuma ya Folorunsho Alakija wa Nigeria) Oprah Winfrey anatarajiwa kutua nchini kwa ziara binafsi.
Kwa mujibu wa taarifa fupi iliyotolewa leo kwa Bongo5 na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ndugu Lazaro Nyalandu, ratiba ya Oprah akiwa nchini bado haijawekwa wazi lakini serikali imeamua kumpeleka kwenda kushuhudia mandhari ya kuvutia katika mbuga ya wanyama ya Serengeti.
“So far, safari yake na ratiba ni water-tight. Tumeamua anakwenda Serengeti kwa ziara binafsi na tumefurahi sana,” Waziri Nyalandu ameiambia Bongo5.
Awali ya hapo, Naibu Waziri huyo alitweet:Oprah Winfrey touring Tanzania this week. Karibu sana dada.”
Pia alizungumzia ujio wa mwanamuziki aitwaye Lynda Turner.
“Mwanamuziki Lynda Turner na mumewe wanatarijiwa kutembelea Serengeti wiki hii. #UtaliiTanzania.”
Previous Post Next Post