NEYMAR AMUITA ROONEY BARCA


rooney2 2ae26
Neymar
rooney 66e98
Wayne Rooney (HM)
NYOTA wa Brazil, Neymar amemtaka mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney kufikiria kuhamia Barcelona, akisema itakuwa ni ndito kucheza na mshambuliaji huyo wa England.
Neymar, ambaye mwenyewe amejiunga na timu hiyo ya Katalunya mapema majira haya ya joto kwa dau la Pauni Milioni 48.6 kutoka Santos ya Brazil, ameitaja Camp Nou kama kituo sahihi kwa mchezaji mwenye kipaji kama Rooney.
Nyota huyo wa Samba, aliyefunga bao wakati Brazil ikiichapa 3-0 Hispania juzi katika Fainali ya Kombe loa Mabara, amesema: "Mtindo wa soka tunaocheza (Barcelona) na viwango vya wachezaji tulionao- ni klabu sahihi kwa wachezaji wakubwa kujiunga nayo,".

 Chanzo: Sportmail
Previous Post Next Post

Popular Items