Ndege ya abiria kutoka Korea Kusini ‘Asiana Airlines’ iliyopata ajali San Fransisco ilikuwa ikiongozwa na rubani aliyekuwa katika “mafunzo” ya kurusha boeing 777



Ndege ya Asiana Airlines kutoka Korea Kusini ilipata ajali jumamosi (July 6) iliyopita wakati ikijaribu kutua katika uwanja wa ndege wa San Fransisco nchini Marekani, na kusababisha vifo vya wanafunzi wawili na kujeruhi wengine zaidi ya 180.

Habari zilizoripotiwa na Reuters zinasema kuwa wakati ndege hiyo ya Asiana inapata ajali ilikuwa ikiongozwa na rubani aitwaye Lee Kang-kook, ambaye alikuwa katika mafunzo ya kurusha Boeing 777 (iliyopata ajali).
Kang-kook alikuwa na uzoefu wa saa 48 tu za kurusha ndege ya 777 kwa umbali mrefu.


Waziri wa usafirishaji wa Korea Kusini Choi Seung-youn alisema hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa rubani huyo kutua ndege aina ya Boeing 777 katika uwanja wa San Fransisco japo amewahi kurusha aina nyingine za ndege mara 29 na kuwa na uzoefu wa jumla ya masaa 9,793 ya kurusha ndege aina tofauti ikiwa ni pamoja na saa 43 ya kurusha 777.


Ajali hiyo ilisababisha vifo vya wanafunzi wawili wa kike kutoka China waliokuwa miongoni mwa kikundi cha wanafunzi 29 waliokuwa katika safari ya mafunzo, na abiria wengine zaidi ya 180 walijeruhiwa katika ajali hiyo.
Previous Post Next Post

Popular Items