Kuna nini kati ya Dr Cheni na Lulu? Dr Cheni ampongeza lulu Michael kwa kuamua kubadilika na kujikita katika kazi.





Baada ya Lulu kutangaza kuwa amebadilika sana toka alipotoka jela, Msanii wa filamu Bongo, Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ amesema anamtakia mafanikio mema kinda la filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kujitangaza kuwa amebadilika.
Akizungumza na paparazi wa GPL, Dk. Cheni alisema  amefurahi kusikia mikakati ya Lulu na kumsihi ajitahidi kuishi hivyo ili aweze kufikia malengo yake kama alivyojipangia.


Cheni amempongeza LULU na amsema anamuombea kwa MUngu ili malengo yake aliyoyaweka yatimie kwani ni jambo zuri sana.
“Kwanza nampongeza na namuombea kwa Mungu atimize malengo yake. Ni jambo zuri kama ameamua kujikita katika kazi zaidi ya kitu chochote,” alisema Dk. Cheni.
news via:GPL
Previous Post Next Post

Popular Items