Ni rahisi sana kubaini ubora wa sauti yake kwenye wimbo huu na hakika Mzee Magali anawazidi uwezo wasanii wengi tu nje huko. Nimependa uamuzi wake wa kuchagua kuimba nyimbo zinazoendana na umri wake na kama watu wakiondoa ile wazungu wanaita Prejudice (mtazamo uliopo awali kwa kuzingatia sababu ama uzoefu), Mzee huyu anaweza kufanya vizuri.
Tusikilize wimbo wake na kuujudge kwa tunachosikia na si kwa kile anachofanya, kwamba kwakuwa anafanya filamu hawezi kuwa muimbaji mzuri. Hata hivyo Mzee huyu anasema muziki ni kitu alichokianza siku nyingi na ana uwezo nacho na huu ni muda muafaka kwake.
Ushauri kwake ni kwamba kama anataka kuendelea, wimbo ujao ajaribu kufanya na studio ama producer mwenye uzoefu zaidi ili wimbo usikike kwa ujazo na ubora zaidi. Kuna kasoro nyingi za kiutayarishaji kwenye wimbo huu hasa kwakuwa unasikika ‘mono’ na haujasambazwa vizuri (panning) kama zitakavyo nyimbo za dance au nyimbo zinazopigwa live.