Hii ndio maana ya tatoo yenye maandishi ya kichina aliyojichora Nicki Minaj.



Onika Tanya Maraj maarufu kama Nicki Minaj member wa Young Money ambaye amezaliwa miaka 30 iliyopita, anasifika kwa style yake ya kurap na jinsi anavyojifananisha na mdoli wa barbie. Kitu kingine ambacho Nicki Minaj anacho ni tatoo ambayo ipo kwenye mkono wa kushoto iliyoandikwa kwa lugha ya kichina. So, umewahi kujiuliza nini maana ya tatoo ile ambayo Nicki Minaj amejichora. Kama ulikuwa hujui ni kwamba hiyo ndiyo tatoo pekee ambayo Nicki Minaj anayo kwenye mwili wake tofauti na boss wake Lil Wayne ambaye karibia nusu ya mwili wake una tatoo.


Kwenye lugha ya kiingereza tatoo hile maana yake ni ”God is always with you”, kwa kiswahili ni kwamba “Mungu siku zote yupo pamoja nawe”. Sources zinasema kwamba Nicki Minaj mwenyewe anasema alijichora hiyo tatoo akiwa na akili za kitoto na kama akiweza kurudi nyuma asingeweza kuichora tena.
Previous Post Next Post