Hali ya Mzee Small inaendelea vizuri na inatia moyo sasa. Michango zaidi inahitajika.




Habari tulizozipata kupitia blogu ya DjChoka zinasema kuwa hali ya Msanii nguli wa maigizo hapa nchini Tanzania, Ndg Said Bin Wangamba almaarufu kama Mzee Smallinaendelea vizuri, na anashukuru sana kwa wale wote wanaomkumbuka katika kipindi hiki kigumu cha maradhi. Kwa sasa anaweza kujikongoja taratibu mwenyewe.,
Habari hiyo inasema kuwa mzee small anaendelea na mazoezi ya kila siku, na kubwa ni dozi ya dawa kwa ajili ya kumsaidia kuondoa uvimbe uliogundulika miezi kadhaa iliyopita, kichwani mwake ambapo dozi moja tu inagharimu takribani 30,000 TZS pamoja na mahitaji mengine ya lazima ya kila siku,
Pia Kwa yeyote atakaeguswa tafadhali unaweza kuwasiliana na Mzee wetu kupitia, M-PESA kwa kutumia namba ya Said Ngamba (Mzee Small) 0754647265 na TIGO PESA kwa kutumia namba ya mkewe 0658111311
Mzee small ni mmoja wa waigizaji nguli sana hapa nchini aliyeleta mchango wa kipekee sana kwenye sanaa ya maigizo upande wa vichekesho hivyo tuzidi kumuombea na kumkumbuka mzee wetu huyu apone haraka.

news via: BongoMovie

Previous Post Next Post