CHELSEA YAUA 4-1, BRUYNE AUMIA GOTI


c 894c8
MSHAMBULIAJI wa Chelsea Kevin De Bruyne akipachika bao la pili la Chelsea. Katika mchezo huo aliumia goti (HM)
c2 ae758
c3 f71d1
CHELSEA imeendeleza rekodi ya ushindi katika ziara yake barani Asia baada ya kuwafunga mabao 4-1 mastaa wote wa ligi ya Malaysia dimba la Shah Alam  , lakini hali imekuwa mbaya kwa kocha Jose Mourinho baada ya kuumia kwa nyota wake Kevin de Bruyne.
De Bruyne alitolewa uwanjani kwa machela baada ya kuumia goti lake wakati akitia kambani bao la pili kwa klabu yake.
Mabao ya Chelsea yalitiwa kambani na Traore (dakika ya 5), De Bruyne ( dakika ya 28), Lukaku (dakika ya 45+4), Moses (dakika ya 88).
Alipoulizwa kuhusiana na majeruhi ya nyota huyo raia wa Ubelgiji, bosi wa Chelsea Jose Mourinho alisema: ‘Wakati akiwa amelala chini na kuomba kufanyiwa mabadiliko, kila mtu katika benchi letu alijisikia vibaya sana”.
Mourinho alisisitiza kuwa katika mechii hiyo, Bruyne ameonesha kiwango cha juu na kumshawishi kila mtu, na hii inaonesha atakuwa mchezaji muhimu katika kikosi chake.
Lakini uchunguzi wa awali haujaonesha kama tatizo ni kubwa sana, hivyo ni matarajio kuwa nyota huyo atarudi mapema uwanjani.
Kikosi cha Chelsea kipindi cha kwanza: Schwarzer; Ivanovic, Terry, Chalobah, Bertrand; Essien, Van Ginkel; De Bruyne (Feruz 31), Traore, Hazard; Lukaku
Kipindi cha pili: Cech; Wallace, Kalas, Cahill, Cole; Ramires, van Ginkel (McEachran 66); Moses, Hazard (Piazon 66), Schurrle; Ba. 

Chanzo: sportsmai
Previous Post Next Post