Wiki ya nane ya shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’ ilikamilika jana (July 21) huku ikiwafungulia mlango Bassey (Sierra Leone) na Pokello (Zimbabwe) ambao ndio waliuga mchezo katika eviction show ya jana.
Bassey
Bassey ndiye aliyekuwa wa kwanza kufahamu hatma yake katika reality show hiyo baada ya kuwa wa kwanza kutajwa kuwa mmoja wa washiriki waliopata kura chache. Cha kusikitisha kwa mshiriki huyo ni kuwa hakua na taarifa kuwa alikuwa katika dangerzone baada ya Bimp kujiokoa kama HOH na nafasi yake kumweka Bassey, na mzambia Pokello ndiye aliyefuatia kutajwa.
Pokello
Baada ya eviction ya jana sasa Zimbabwe na Sierraleone zimetoka rasmi katika shindano hilo sababu washiriki wao wote wameshatoka na kufanya idadi ya washiriki 16 ambao tayari wameshatoka. Mpaka sasa ni Tanzania pekee nyio imebaki na washiriki wote wawili huku jirani zetu Kenya wamebaki na mshiriki mmoja ambaye ni Annabel.
Afrika Mashariki imezidi kuthibitisha kuwa linapokuja swala linalohusu moja ya nchi hizo mashabiki wanakuwa kitu kimoja na kumpigia kura muwakilishi wa moja ya nchi hizo. Tanzania na Uganda kwa mara nyingine ziliungana na Kenya kumuokoa Annabel kwa mara nyingine aliyekuwa katika kikaango cha ‘Biggie’.
Leo mchezo huo unaingia wiki yake ya tisa zikiwa zimesalia wiki chache tu kufikia siku ya fainali itakayomuweka hadharani mshindi wa $300,000. Endelea kuwapigia kura washiriki wa Tanzania ambao bado wana nafasi kubwa ya kuishangaza Afrika katika msimu wa nane wa Big Brother The Chase.
Hivi ndivyo kura zilivyopigwa katika wiki ya nane iliyokamilika jana (July 21)
Angola: Angelo
Botswana: Angelo
Ghana: Pokello
Kenya: Annabel
Ethiopia: Dillish
Malawi: Dillish
Namibia: Dillish
Nigeria: Bassey
South Africa: Angelo
Sierra Leone: Bassey
Tanzania: Annabel
Uganda: Annabel
Zambia: Angelo
Zimbabwe: Pokello
Rest of Africa: Angelo
Botswana: Angelo
Ghana: Pokello
Kenya: Annabel
Ethiopia: Dillish
Malawi: Dillish
Namibia: Dillish
Nigeria: Bassey
South Africa: Angelo
Sierra Leone: Bassey
Tanzania: Annabel
Uganda: Annabel
Zambia: Angelo
Zimbabwe: Pokello
Rest of Africa: Angelo
Total: Angelo = 5; Annabel = 3; Dillish = 3, Pokello = 2, Basssey = 2. (Total: 15 Votes)