Mashindano yanayoendeshwa na kituo cha East Africa TV na Radio kwa kudhaminiwa na kampuni ya simu ya Mkononi ya VodaCom yafikia hatua ya nusu fainali.
Mashindano ya dancer miamia yalianza na makundi 60 na hadi hivi sasa makundi 15 yatinga nusu fainali.
Mshindi wa dancer miamia kuibuka na kitita cha milioni 5 za kitanzania na makundi yaliyotinga nusu fainali ni
Mabaizo, Makaba, Ganzi more fire, The choclate, DDI Crew, The WT, Best fiend, The winners, Get dancerz, Ikulu Vegas,World Chmpion, Mazaba powder, Wakali sisi, Pambana squad pamoja na Take over.
Mashindano hayo yataendelea katika hatua ya nusu fainali tarehe 18 august mwaka huu katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay.