ARSENAL YAFUFUA MPANGO WA KUMSAJILI FABREGAS


fab 0da20
Cesc Fabregas huenda akarudi Arsenal baada ya timu hiyo kufufua matumaini ya kumsajili (HM)

fab2 c0976

KWA mara nyingine Arsenal inataka kumrejesha Nahodha wake wa zamani,Cesc Fabregas majira ha ya joto.
Kwa sasa kiungo huyo wa zamani wa The Gunners yupo mapumzikoni baada ya kumaliza kuichezea Hispania kwenye Kombe la Mabara na mustakabali wake Barcelona haueleweki kutokana na msimu mbaya uliopita.
Taarifa nchini Hispania zimeendelea kusema atabaki Nou Camp, lakini shaka inaletwa na namna atakavyoingia kwenye mipango ya kocha Tito Vilanova baada ya msimu uliopita kutemwakatika mechi zote kubwa.

Dili la kumsajili tena Fabregas halitakuwa na utata, kwa sababu wakati Arsenal inamuuza mchezaji huyo Hispania kwa Pauni Milioni 25, ilipewa nafasi ya kwanza ya kumsajili ikimhitaji.
Ikiwa Barca itaamua kumuuza Fabregas, The Gunners watapewa nafasi ya kwanza ya kumsajili kwa Pauni Milioni 25.
Previous Post Next Post