VICTORIA KIMANI KUTOKA KENYA KUTUMBUIZA KWENYE SHOW YA BIG BROTHER WIKI HII



Ikiwa imebaki siku moja kuifikia siku ya eviction katika shindano la Big Brother ‘The Chase’ huko Africa Kusini, tayari imefahamika kuwa dada wa rapper wa Kenya Bamboo aitwaye Victoria Kimani atatumbuiza katika show hiyo.
Binti huyu mrembo ambaye pia amekua nominated katika tuzo za Nigeria Entertainment Awards 2013 katika kipengele cha the Most Promising Female Act zinazotarajiwa kufanyika New York, Marekani baadae mwaka huu, atasindikiza show hiyo Jumapili (June 9) ambayo itawapa jibu watanzania juu ya hatma ya mshiriki Feza Kessy ambaye yuko katika danger zone wiki hii.
Kimani ambaye muda wake mwingi amekuwa akifanya shughuli zake nchini Kenya, Nigeria na Marekani ameshafanya kazi na wanamuziki wakubwa duniani kama Busta Rhymes, Chris Brown na wengine.
Previous Post Next Post

Popular Items

Magazetini Ijumaa ya Tarehe 23/8/2013