Mashabiki wa mchezaji mstaafu wa Uingereza David Beckham wa nchini china wamejeruhiwa katika vurugu zilizotokea wakati wa mapokezi ya nyota huyo nchini China. Beckham yuko China kwa ziara ya wiki moja akiwa kama balozi wa soka la nchi hiyo.
Kwa mujibu wa The Guardian watu wapatao saba walijeruhiwa baada ya umati wa mashabiki wapatao 1000 kusukumana wakati wa mapokezi ya star huyo katika chuo cha Tongji nchini China. Kati ya waliojeruhiwa wamo maaskari watatu, walinzi wa chuo cha hicho wawili na wanafunzi wawili.
Inasemekana umati huo mkubwa ulikuwa umekusanyika katika uwanja wa chuo hicho ambapo Beckham alipangiwa kwenda kukutana na team ya chuo. Baada ya vurugu hizo kutokea zoezi zima lililokuwa limepangwa liliahirishwa.
Wakati Beckham anawasili uwanjani hapo mashabiki hao waliokuwa na kiu cha kumuona kwa karibu walivamia geti na kuwazidi nguvu walinzi wa uwanja pamoja na maaskari, kitendo kilichopekea mkanyagano uliosababisha watu kujeruhiwa.