TEVEZ ATUA JUVE KWA PAUNI MILIONI 10


tevez2 89057
Carlos Tevez
tevez 33b59
MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Carlos Tevez anajiandaa kuhamia Juventus baada ya klabu hizo mbili kukubaliana kuuziana mchezaji huyo kwa ada ya Pauni Milioni 10.
Viongozi wa mabingwa hao wa Serie A walisafiri hadi Uingereza usiku wa jana kukamilisha dili la kumchukua Muargentina huyo.
Tevez alikaribia kuondoka vibayakipindi cha nyuma City na sasa inatokea ataondoka vizuri Etihad baada ya makubaliano ya kumuuza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amebakiza mwaka mmoja Etihad na anaweza kuondoka bure katika klabu hiyo msimu ujao.
Tevez anatarajiwa kwenda Turin kufanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha usajili huo. Chanzo: binzubeiry
Previous Post Next Post