RONALDO KURUDI MANCHESTER UNITED KWA PAUNI MILIONI 65..



Paundi miloni 65 zaandaliwa kumrejesha Old Trafford, akataa kusaini mkataba mpya Madrid

MANCHESTER UNITED imepiga hatua katika jitihada zake za kumsaini tena Cristiano Ronaldo.
United imetenga pauni milioni 65 pamoja na mchezaji ili kumnasa supastaa huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye bado anachukulikwa kama shujaa ndani ya Old Trafford.
Inaaminika kuwa Ronaldo pia anataka kurejea Manchester United.
Amekataa ofa ya kusaini mkataba mpya Real Madrid huku mkataba wake wa sasa ukiwa umebakiza miaka miwili.
Real Madrid nao wanaandaa pauni milioni 80 kwaajili ya usajili wa Gareth Bale iwapo Ronaldo atatimka.
Ronaldo ambaye kwa siku za karibuni amekuwa hana raha ndani ya Real Madrid, ameiweka sokoni nyumba yake iliyoko Madrid na hakucheza mchezo wa mwisho wa timu hiyo baada ya kuzinguana na kocha Jose Mourihno.
source:thesun 
Previous Post Next Post