Quick Rocka aongelea Juu ya kupitia Clouds E kuhusu project yake mpya aliyofanya na marehemu Mangwair



Kupitia Clouds E ya Clouds TV jana rapper kutoka Mbeya Quick Rocka amefunguka juu ya ngoma yake mpya inayokuja tarehe 31 mwezi huu pamoja na video yake.
Kwenye interview Quick Rocka amesema, “it’s almost a year now tangu nitoe kazi kwa watu wangu. Sasa hivi nimekuja na kitu kinaitwa my baby ndani yake yupo the late CowObama na Shaa. Tarehe 31 mwezi huu ndiyo nitaiachia ngoma na video yake pamoja. My plans ni kufanya launching kwenye kiota kimoja wapo cha starehe na ofcoz utaiona trailer/teaser ya video yenyewe hapahapa kupitia Clouds E.”
Kuhusu sehemu ya Mangwair kwenye video hiyo, Quick amesema: “Sehemu ya Mangwair verse yake itakuwepo kama kawaida, kuna replacement nzuri ambayo tunaamini watu wataipenda tumeifanya hapo. So, what is it na nini tutafanya let it be suprise video ikitoka.”
Clouds E (all entertainment news) huoneshwa kila siku saa mbili usiku kupitia Clouds TV.
Previous Post Next Post