Picha: Show ya Mwana Fa The Finest - June 14 2013








Mwana FA akiwasili katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam huku akiwa amevalia suti matata iliyotengenezwa na mbunifu wa mavazi anayekuja kwa kasi nchini Sheria Ngowi.




Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA akikamua jukwaani wakati wa Show ya Kijanja ya The Finest iliyorindima usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar. Nyuma yake ni Msanii Linah aliyeshirikishwa kwenye nyimbo ya YALAITI aliyoimba na Mwana FA akisubiri kutumbuiza.





Msanii wa muziki wa Bongo Flava nchini Ben Paul akisindikiza kutoa burudani wakati wa show ya Mwana FA iliyopewa jina la “The Finest”. Wasanii wote walionekana nadhifu kwa kuvaa masuti ya gharama.




Kutoka (kulia) ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe, akiwa na Mbunge wa Bumbuli (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba, wakiwa ni miongoni mwa mashabiki wa Mwana FA, waliohudhulia shoo hiyo. Kushoto ni Mtangazaji wa Clouds FM, Gerald Hando.




Mashabiki wa Mwana FA, wakimshangilia Superstar wao wakati akitoa burudani.




Mrembo wa Wema Sepetu na Kidate wake nao walikuwepo kwenye show ya wajanja.




Mashabi wa Mwana FA wakionekana kukongwa mioyo yao wakati wa show iliyobeba jina la “THE FINEST”…Na kweli ilikuwa The Finest kama inavyoonekana pichani.


Watu weweeeeeeeeeee…..ukumbi ulirindima Shangwe za mashabiki wa Mwana FA.




Mwana FA akiendelea kuwapa raha mashabiki wake.


Wadau wakishow love nje ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.



Gerald Hando.

Mashabiki wa Mwana FA, wakimshangilia Superstar wao wakati akitoa burudani.

Mrembo wa Wema Sepetu na Kidate wake nao walikuwepo kwenye show ya wajanja.

Mashabi wa Mwana FA wakionekana kukongwa mioyo yao wakati wa show iliyobeba jina la “THE FINEST”…Na kweli ilikuwa The Finest kama inavyoonekana pichani.


Asma Makau, Jojo, Shadee & Afriend wakiwa nje ya ukumbi wa makumbusho ya Taifa Dar es salaam kwaajili ya kuingia ndani kushuhudia 'The Finest'. 




Vanessa Mdee na B Dozen katika viwanja vya Makumbusho kabla ya 'The Finest' Show 


Halima Kambi, Dar.

KATIKA Shoo hiyo ya ‘Kijanja’ pia ilihudhuriwa na wasomi kibao huku baadhi ya wabunge kama Mh. Zitto Kabwe na January Makamba wakiwa ni miongoni mwa mashabiki wajanja waliohudhuria katika shoo hiyo ya “kijanja” ya ‘The Finest’ iliyofanyika katika Ukumbi Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.

Mwana FA, pia alisindikizwa na na baadhi ya wasanii kama, Ben Paul, Linah, Maua, Dully Sykes na wengine kibao pamoja na bendi ya Njenje

Kiukweli show ilifana sana kutokana na utaratibu na mpangilio na maandalizi ya shoo yenyewe na MwanaFA aliweza kufanya yake jukwaani na kuwapagawisha mashabiki wake katika usiku ule.
Previous Post Next Post