ORIJINO KOMEDI WAULA,WAINGIA MKATABA MNONO WA USIMAMIZI WA KAZI ZAO.




  Mkuu wa kitengo cha Vipaji na Uendelezaji wa Biashara kutoka  ROCKSTAR4000,Christine “Seven” Mosha , akifafanua jambo mbele ya Wanahabari kwenye mkutano wao uliofanyika jijini Dar kuhusiana na Kundi la kipaji cha televisheni “Orijino Komedi”  kuingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency kwa  kushirikiana na Rockstar 4000.
 Pichani shotoni ni Mpoki akizungumza machache kwenye mkutano huo, kati ni Joti na  Mkurugenzi mkuu wa Nexus, Bwana Bobby Bharwani
 kutoka kushoto ni Mpoki, Joti, Bobby, Seven, Seki, Masanja na Maclegan
Mpoki, Kitenge, Maulid, Joti, Seki, Masanja na Maclegan

=========== ====================

KUNDI LA KIPAJI CHA TELEVISHENI KINACHOONGOZA TANZANIA 
 ORIJINO KOMEDI WASAINI MKATABA MNONO WA USIMAMIZI 

Kundi la kipaji cha televisheni “Orijino Komedi” linaloongoza nchini kwa vipindi vyake  kupitia television imeingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency kwa  kushirikiana na Rockstar 4000. Mkataba huu unakuwa wa kwanza kwa wasanii wa  luninga kupitia kampuni hii ya Nexus

Nexus imenunua haki zote za usimamizi wa biashara na uongozi wa kundi hilo ambalo  linajulikana sana nchini kupitia vichekesho vyake kupitia vituo vya televisheni na  matamasha mbali mbali ambapo mkataba huu utakuwa ni kwa ajili ya kusimamia kipindi  hiki cha vichekesho kinachoundwa na wachekeshaji saba wajulikanao kama; Joti,  Maclegan, Masanja, Wakuvanga, Mpoki, Vengu na David Seki ambacho kimekuwepo  hewani kwa mfululizo wa miaka sita.

 Kushirikiana na Orijino Komedi ni kitu cha muhimu kwa Nexus kwani siku zote  imekuwa ikitamani kufanya kazi kwa karibu na kundi hilo na kuthamini kazi zao  kutokana na vipaji vya hali ya juu walivyokuwa wakionyesha wasanii wa kundi hilo;  alisema Mkurugenzi mkuu wa Nexus, Bwana Bobby Bharwani. 

“Nimefurahishwa sana kufanya kazi na watu wenye vipaji vya hali ya juu na kuiingia  mkataba na Kampuni ya Nexus Agency. Kwa pamoja tumedhamiria kukuza na  kubadilisha dhama ya vipaji na sanaa kutoka ilipo na kuwa ya kimataifa” alisema  Christine “Seven” Mosha , Mkuu wa kitengo cha Vipaji na Uendelezaji wa Biashara kutoka  ROCKSTAR4000.

Muandaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni Davis ‘Seki’ amesema wanafuraha  kuingia mkataba wa kazi na kampuni ya Nexus Agency na Rockstar 4000 Africa, mbapo ameahidi kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kukidhi haja ya soko.

Kwa kushirikiana na Rockstar 4000, nexus inatambua na kuthamini vipaji hivyo  itahakikisha inaendeleza vipaji vya wasanii wa kundi hilo ili vipaji vyao viweze kufikia  kiwango cha juu vya ufanisi ndani ya Afrika na kimataifa kwa ujumla. 

Jiunge na kufuatilie Orijino Komedi kwenye:
Website 
www.orijinokomedi.com
YouTube
www.youtube.com/orijinokomedi
Twitter
www.twitter.com/orijinokomedi
Facebook
Previous Post Next Post