MAMIA WA MASHABIKI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA WAJITOKEZA KUPOKEA MWILI WAKE HUKU WENGINE WAKIIMBA NYIMBO ZAKE NA KULITAJA JINA LAKE! WENGINE WALIA KWA UCHUNGU. [PICHA]



Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam wakiwemo wasanii wa muziki na filamu nchini leo wamejitokeza kuupokea mwili wa marehemu Albert Mangwea kwenye uwanja wa ndege wa Mwl Julius Nyerere uliowasili kutoka nchini Afrika Kusini.




Wasanii Dollo na KR Mulla

Bongo5 imeshuhudia umati mkubwa wa mashabiki wa Mangwea aliyefariki wiki iliyopita nchini humo uliokuwa na hamu kubwa ya kushuhudia jeneza lililokuwa na mwili wake.Baadhi ya vijana waliokuwa wakiiimba kwa sauti waliizingira gari iliyokuwa na mwili na kutaka walibebe jeneza kwa mkono na hivyo kuufanya msafara uliokuwa ukielekea kwenye hospitali ya Muhimbili usimame kwa muda bila kusogea.




Umati wa watu ukisubiri kuona gari lililobeba mwili wa Mangwea







Umati wa watu ukisubiri kuona gari lililobeba mwili wa Mangwea

Umati wa watu ukisubiri kuona gari lililobeba mwili wa Mangwea




Vijana hao ambao wengine walionekana wakilia kwa uchungu wamesikika wakiimba ‘Tumshushe, Tumbebe’.

Hali hiyo imepelekea kuzuka kwa vurugu iliyowapa wakati mgumu polisi waliosambazwa kuangalia hali ya usalama.

Wasanii mbalimbali wameonekana wakipokezana kubeba msalaba kuliongoza gari lililobeba mwili baada ya wananchi kuwataka washuke kwenye magari.

Mtangazaji wa Times FM, JABIR SALEH Ametweet: P funk ameamua kukimbia na kutembea na wana ili folen iende!!!much lov kwa p anakimbia hadi anatia huruma!”

Umati wa watu ukisubiri kuona gari lililobeba mwili wa Mangwea


Mkoloni na Profesa Ludigo

Fid Q alikuwa mmoja ya wasanii waliojitokeza

Hafsa Kazinja na Quick Rocka wakiwa na simanzi

Chege


Abdul Kiba, Hafsa Kazinja na Sauda Mwilima

Izzo B akiwe mwenye majonzi makubwa

Mrisho Mpoto








Mwili wa Mangwea ukiwa umebebwa




Dr Cheni
Previous Post Next Post