Interview na Cathy wa Bongo Movies, aongelea vifo vya wasanii na mambo ya uchawi ndani ya bongo movies





Jana tarehe 18/06/2013 tuliweza kupata nafasi ya kufanya interview na mwigizaji cathy toka club ya bongomovies kwa njia ya simu kuhusu mambo kadhaa juu ya tasnia ya Filamu nchini.

Moja ya maswala tuliyozungumza naye ni kuhusu vifo mbalimbali vinavyotokea kwa wasanii wa mbalimbali nchini na tuhuma za uchawi zinahusiana na vifo hivi.

Tuliamua kufanya naye interview hii baada ya blog moja maarufu nchini kuripoti taarifa za yeye kuongelea mambo hayo na sisi tuliamua kutafuta ukweli Zaidi wa stori hii na kilichoandikwa kwenye blog hiyo.

Maongezi yalikuwa hivi:

Bongo61: Mambo cathy mzima?

Cathy: Mzima jamani, kwema?

Bongo61: Kwema kabisa, vipi mishe mishe?

Cathy: Namshukuru Mungu kwakweli, kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa.

Bongo61: Tumesoma stori moja leo kuhusu interview yako na blog moja hivi maarufu nchini, na inasema umesema wasanii wapunguze uchawi!!? Vipi tena?

Cathy: Mmmh!, sikumbuki hiyo interview, ila kuna mtu mmoja alinipigia simu na kunitania kuhusu uchawi ndani ya tasnia ila sikumbuki kufanya hiyo interview.

Bongo61: Ila unazungumzijae masuala ya uchawi kwenye tasnia yetu hii?

Cathy: Binafsi siamini kama kuna hayo mambo jamani, na sielewi watu wanaoamini wanafikiria nini, naona ni upumbavu na upotezaji wa muda tu.

Bongo61: Inaamaana huamni kabisa kuwa uchawi upo au?

Cathy: Siamini, na siamini kama kuna mtu anaweza kuniroga kama wanavyosema, hayo mambo ni ujinga tu na yanarudisha maendeleo nyuma.

Bongo61: Vipi kuhusu masuala ya wasanii kufariki na watu kuhusisha vifo hivyo na mambo ya uchawi?

Cathy: Unajua mi nashangaa sana, watu wanakufa kila siku, sema kwasababu hawajulikani ndo maana jamii inaona hawana maana. We jaribu kwenda muhimbili siku moja uangalie ni maiti ngapi zinapita pale mochwari ndo utajua ni watu wangapi wanakufa. Mi naamini kuwa mtu anakufa siku zake za kuishi zinapoisha, na sio mambo mengine. Wasanii wamefariki kweli, akiwemo rafiki yangu Kashi, na nimehuzunika sana sana ila siamini kama ni uchawi. Na vifo vyao kufuatana inawezekana ndio walivyopangiwa hivyo, mbona watu wengi wanafariki huko duniani kila saa, tutasema na huko ni uchawi??? Tuache fikra potofu jamani

Bongo61: Ila watu wengi wamekuwa wakilalamikia haya mambo ya kuuana hasa kwa nyie mastaa, we huoni kama kuna kunaweza kuwa na ukweli ndani yake?

Cathy: Ngoja nikwambie kitu kimoja, mi naamini katika Mungu, na naamini yeye ndo mwanzo na mwisho. Hayo ya uchawi mi siyaamini na sitaki kuyafuatilia, kila mtu ataongea la kwake, ukianza kufuatilia utajikuta huna la kufanya

Bongo61: Na unashauri nini kifanyike labda au tujifunze nini kupitia matatizo haya?

Cathy: Tumrudie Mungu jamani, kuwa staa isiwe sababu ya sisi kufanya mambo ya kishenzi. Tujenge heshima ili hata siku tutakapofariki, tufariki kwa heshima na sio vinginevyo

Bongo61: Basi tunashukuru sana kwa muda wako huu wa kuongea nasi

Cathy: Wala msijali, muda wowote mi nipo hapa kama kuna lolote usisite kuniambia

Bongo61: Kazi njema na siku njema

Cathy: Asanteni sana

Previous Post Next Post