WALE WASANII WATAKAOTUMBUIZA KWENYE UFUNGUZI WA BIG BROTHER AFRICA WATAJWA



Show ya ufunguzi wa msimu mpya wa shindano la Big Brother Africa itafanyika Jumapili hii, May 26 nchini Afrika Kusini. Usiku huo utawaonesha washiriki wote 28 watakaoanza safari ya miezi mitatu ya kuzisaka dola laki tatu za msimu wa nane wa Big Brother Africa, The Chase.


Miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye ufunguzi huo ni pamoja na STL wa Kenya, Don Jazzy, D’ Prince na Wande Coal kutoka Nigeria na kundi la Mafikizolo la Afrika Kusini.


Pia mchekeshaji wa Kenya Daniel Ndambuki, maarufu kama Churchill atapanda kwenye stage kuwavunja mbavu watazamaji wa show hiyo katika nchi 50 barani Afrika. Show hiyo itaonekana live pia kupitia website ya Big Brother, www.bigbrotherafrica.com.
Previous Post Next Post