Vijana 10 chini ya miaka 30 kwenye muziki, fashion na habari Tanzania wa kuwaangalia 2013




Miongoni mwa vijana hawa kumi hujawahi kuwasikia kabisa lakini kuwa na uhakika kutoka kwetu kuwa ni vijana wachapakazi, wabunifu, wana malengo makubwa na wengine tayari ni ma CEO wa makampuni yao wenyewe. Cha kufurahisha zaidi ni kuwa wote hawa wana umri chini ya miaka 30. Bila wasiwasi, hawa ni miongoni mwa vijana wa kuwaangalia sana mwaka 2013 na kuendelea.

Gavin Gosbert aka Soul Kid


Gavin aka Soul Kid anatokea Arusha na alizaliwa miaka 26 iliyopita.Ni mpiga picha aliyejifunza kwa utundu wake mwenyewe. Ni msanii wa graphics na pia ni cinematographer.Pia Gavin ni producer wa muziki na mpiga gitaa hodari.

“I am thankful to God for gracing me with the opportunity to establish my very own company with my colleague Melchizedech, registered as Black n White Visual Studios. Throughout the year I’ve had the chance to work with many clients like, Teenspot magazine, Paa magazine, Dar Life magazine and Clouds Media company.

I have also worked with Africare NGO and Orca-Deco furniture store. I have worked with beautiful people in the fashion industry; Miss Universe last year Nelly Kamwelu, Miss Universe this year the beautiful Winifreda, Miss world Tanzania this year Lisa Jensen, Miss University Africa Tanzania this year the enthusiastic Hamisa Mobeto, Miss Tanzania 2006 1st runner up Jokate Mwigelo and a lot other models.

I’ve also got into the Music video and short film industries and had a chance to become the co director and cinematographer of two music videos; Amatita by Pah one and Nichumu by Bob Junior both of which I co-directed with Eryne Epidu.

I’m honored to have met wonderful people like Andrew Mahiga, Amin `Swai, Vanessa Mdee, Jokate Mwigelo, Maria Sarungi, Lisa Jensen and a lot more who have inspired me in many ways in all walks of life.”

Dennis Herman aka Kapwipwi


Dennis Herman aka Kapwipwi ni mchoraji mwenye kipaji na uwezo mkubwa. Amesomea kwenye chuo cha sanaa cha Bagamoyo. Kazi alizozifanya ni pamoja na kuchora picha zote kwenye kitabu cha watoto cha Nancy Sumari, Nyota Yako. Pia amekuwa akichora picha kadhaa kwaajili ya Bongo5 na jarida la Mzuka. Hii ni miongoni mwa picha alizozichora kwenye jarida la Mzuka.


Osse Greca Sinare


Osse Greca Sinare ni mpiga picha wa fashion aliyeshinda tuzo ya ‘Fashion Photographer of the Year 2012’ ya Swahili Fashion Week. Pia jarida la Teenspot lilimtaja kwenye orodha ya ‘10 Most Powerful Youth in Tanzania for 2012.’

Osse ni mwanzilishi na mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya OGS Multimedia studio inayojihusisha na upigaji picha na utengenezaji wa graphics. Kupitia kampuni yake, Osse ameshafanya kazi na makampuni kama Akemi | Tanzania’s Revolving Restaurant, Precision Air In-flight Magazine, Vodacom, Hassan Maajar Trust, Bang Magazine, Bank M, Maznat Bridal Salon na pia akiwa kama mpiga picha wa Teenspot Magazine.

“My work is inspired by many things I experience and see from day to day activities. I could see an abandoned apartment or children playing in the playground and it would instantly trigger an idea for me to try out. I always spend countless hours on-line searching for inspiration from other artist and magazines for constant inspirations.

The type of photography that inspires me is high end fashion, and vintage, dreamy almost surreal. I love all the different beauty you can find in people and love sharing that with others in my photos.

I pride my work not on the technical ability but more on my creativity and the valuable people that contribute to my ideas. I love the whole process of the idea creation to the finish of a project, it truly excites me. Photography is my passion and always will be.”

Pedaiah Swank John


Pedaiah ni model wa kitanzania anayekuja kwa kasi nchini aliyezaliwa March 7th, 1990. Amehitimu shahada ya Software Engineering mwaka 2012 nchini Malaysia. Ameshafanya matangazo mengi ya biashara ya makampuni makubwa nje na ndani ya nchi. Hivi karibuni alianzisha mavazi yake ya PSJ Couture.

Lengo lake ni kuwa model na mbunifu wa mavazi wa kimataifa.

“My passion is fashion & modelling since childhood after I started my university life that’s when I started working with a number of photographers been enjoying every moment since then. This page showcases some of the work which I have done with different photographers.”


Nisher


Nisher ni muimbaji, mwandishi wa nyimbo, graphics designer, mtayarishaji wa muziki, muongozaji na mtayarishaji wa video za muziki, mpiga picha na fani nyingine. Afahamika kwa kutayarisha video za wasanii kama Joh Makini, G-Nako, Mabeste, Bonta, Belle 9 na wengine. Hivi karibuni amefanya video ya Feza Kessy ya wimbo wake Amani ya Moyo na Jikubali ya Ben Pol.

Andrew Mahiga


Andrew Mahiga ana umri wa miaka 26. Ni mkurugenzi mtendaji wa asasi isiyo ya kiserikali ya masuala ya habari, Maanisha Foundation, ambayo lengo lake ni kuwashawishi vijana kubadilisha jinsi wanavyofikiria na kujihusisha kwenye biashara zenye mafanikio.

Maanisha Foundation ina lengo la kuwapa taarifa vijana wa Tanzania ili waamke kutafuta fursa kwaajili ya kujiendeleza wao wenyewe na Tanzania kwa ujumla kupitia televisheni, radio, magazeti na website. Andrew na timu yake wana nia ya kuifanya Maanisha kuwa chombo cha habari chenye magazeti na majarida yake na vipindi vyake vya radio na televisheni.

Tayari wana kipindi chenye mafanikio cha Temino kinachorushwa kupitia Clouds FM. Andrew Mahiga, ana Bachelor of Art – (International Studies) aliyoipata New York , Marekani. Wakati anasoma alifanya field kama mwandishi wa makala za mtandaoni kwenye jarida la Complex Magazine. Ameshafanya kazi pia kwenye kampuni ya Push Observer Media Monitoring. (Daily News).

Hamisa Mobeto


Hamisa Hassani Mobeto alizaliwa mwaka 1994 mkoani Mwanza na kabila lake ni Mnyamwezi. Alianza kufahamika baada ya kushinda taji la Miss XXL BACK TO SCHOOL BASH mwaka 2010 iliyoandaliwa na kipindi cha XXL kutoka Clouds FM.

Nyota yake ilianza kung’ara mwaka 2011 baada ya kuibuka mshindi wa pili Miss Dar Indian Ocean, mshindi wa pili Miss Kinondoni na kuingia nusu fainali ya Miss Tanzania mwaka huo wa 2011.

Hamisa amejipatia mafanikio makubwa kupitia fani ya uanamitindo na uigizaji ambapo ameshiriki kwenye maonesho mengi sana ya mavazi na filamu tofauti nchini.

Amekuwa kivutio kikubwa kwa wasichana wengi wa kitanzania na kumfanya role model wao wengi wakipenda siku moja kuwa kama yeye.

Pamoja na hayo yote Hamisa ana ndoto za kuja kuwa mmoja kati ya wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa hapa Tanzania. (http://zeddylicious.blogspot.com)

Perfect Crispin


Kama umewahi kusikiliza kipindi cha Club 10 na cha Clouds FM, jina la Perfect si geni kwako. Ni kijana mdogo mwenye uwezo mzuri hewani. Uchangamfu wake kwenye radio, umekifanya kipindi chake kuwa miongoni mwa vipindi vya wanafunzi vinavyovutia na vyenye wasikilizaji wengi.

Kenedy the Remedy


Frank Orio ama kama anavyojulikana zaidi kwa jina la Kenedy “The Remedy” ni mwandishi wa habari ameshafanya kazi kwenye tasnia ya habari kwa kipindi cha miaka minne. Ni mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha Saturday Hotmix cha East Africa Radio.

Anafahamia zaidi kwa segment ya habari za burudani kwenye kipindi cha The Cruise na Mishemishe Za Wiki kwenye kipindi cha Planet Bongo.

Doreen E.K.P. Noni


Kama ulikuwa hufahamu ni kwamba Doreen ndiye mbunifu wa mavazi anayewavalisha washiriki wa shindano la Bongo Star Search. Doreen Estazia Kang’wa Peter Noni, alizaliwa miaka takriban 25 iliyopita jijini Dar es Salaam. Ameshabuni pia mavazi ya waigizaji wa tamthilia ya Siri ya Mtungi. Baba yake, Peter Noni anatokea Bupandagila, Mwanza na mama yake Machame, Moshi.

Amesoma Nottingham Trent University nchini Uingereza na kutunukiwa Bachelor of Arts (Hons) in Multimedia with specialization in Animations & 3D Visualization. Mwaka 2008, Noni alianzisha fashion brand label, Eskado Bird iliyopata mafanikio makubwa nchini.
Previous Post Next Post