TAMASHA LA KUMKUMBUKA BOB MARLEY KUFANYIKA RWANDA




Wasanii mbalimbali nchini Rwanda Kigali wanatarajia kuungana kwa pamoja jijini humo kwa ajili ya sherehe ya kumuenzi na kumkubuka aliyewahi kuwa gwiji nyota wa miondoko ya Reggae duniani, Nesta Robert “Bob” Marley,

Tamasha hilo ambalo linatarajiwa kufanyika kuanzia siku ya Ijumaa na Jumamosi hii ambayo ni tarehe 11 ya mwezi huu, ni kumbukumbu ya siku aliyofariki gwiji huyo ambapo itakuwa ni siku muhimu kwa wapenzi wa miondoko hiyo kuungana katika tamasha hilo kubwa na la aina yake.
Aidha wasanii ambao wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo wamo Jah Bone D ambaye ni mzaliwa wa Rwanda mwenye makazi yake nchini Switzerland, Jay Polly, Jean Paul Samputu, Natty Dread na Sophia Nzayisenga na wengineo ambao watatumbuiza katika sherehe za kukumbukwa kwake gwiji huo aliyezaliwa tarehe 6 ya mwezi Februari mwaka 1945 na kufariki tarehe 11 Mei mwaka 1981 kwa ugonjwa wa saratani.
Previous Post Next Post

Popular Items