Roma awadiss viongozi wanaotumia Kiingereza kingi kwenye mitandao ya kijamii






Ameandika Hivi:

Kwanini viongozi wetu wa serikalini wengi wao na mara nyingi sana, WANA TWEET KWA LUGHA ZA KIGENI? Yaani kingereza, wanaandika status zao kwa lugha za kigeni yaani Kiingereza na hata baadhi ya mahojiano yao wanatumia lugha hiyo hiyo ya Kiingereza sio wote na sio mara zote.Lakini je ni kwanini wanafanya hivo? KUNA UMUHIMU WA HILI NCHINI KWETU? WAKATI WANACHOKIONGEA KINAMUHUSU BIBI YANGU KULE

-MPUI SUMBAWANGA
-NANJILINJI
-LUSANGA -MUHEZA
-KICHEBA
NA YEYE HAJUI LUGHA HIYO!!!

Nyerere aliwahi sema:”KITU UKIKIONGEA KWA KINGEREZA HUONEKANA KINA MAANA SANA!!LAKINI KUMBE PENGINE HAKINA HATA MAANA BASI TU TUNAOGOPA WANAVYOTAJA PARLIAMENT haraka haraka!!!

WATANZANIA WENGI HAWAWAELEWI!!!
Previous Post Next Post