NEEC NA UDEC YATOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WALIOHITIMU VYUO VIKUU NA KUKOSA KAZI STADI ZA KUJIAJIRI




Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Annacleti Kashuliza akifungua mafunzo ya wiki 3 ya Vijana 40 waliohitimu masomo ya elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam miaka ya hivi karibuni ambao hawana kazi leo jijini Dar es salaam .Mafunzo hayo kwa vijana yanalenga kuwajengea uwezo wa kuanzisha miradi ya maendeleo na kuwafanya waweze kuajiri vijana wengine pamoja na kusaidiwa kupata fedha benki kwa 
ajili ya kuanzisha biashara kutokana na michanganuo watakayoiwasilisha.



Sehemu ya Vijana 40 waliohitimu katika chuo Kikuu cha Dar es salaam miaka ya hivi karibuni ambao hawana ajira wakiwa katika mafunzo ya wiki 3 ya kuwajengea uwezo wa kuweza kujiajiri wenyewe kwa kuanzisha miradi itakayowajengea uwezo wa kuajiri vijana wengine. Mafunzo hayo yanayoendelea katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam sehemu ya Biashara yameandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) na Kituo cha masuala ya Biashara na uchumi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDEC) ikiwa ni moja ya mkakati wa kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana wa vyuo vikuu nchini. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Previous Post Next Post

Popular Items