NAZIZI AHAMISHA MAKAZI




Taarifa zilizosamba mtaani kwa sasa zinaweka wazi kuwa, Rapa mkongwe wa kike katika game la muziki nchini Kenya, Nazizi, baada ya kufanya makazi yake huko Lamu kwa muda mrefu, sasa ameamua kurejea tena Jijini Nairobi.

Katika mahojiano ambayo amefanya hivi karibuni, Nazizi pia ameahidi kuwa, Ujio wake Nairobi pia utaongeza kasi ya kazi za muziki wanazo piga na Wyre wakiwa kama Necessary Noise, ingawa pia kazi zao za binafsi zitakuwa zikiendelea.

Ujio wa rapa huyu Jijini Nairobi ni hatua ambayo pia inaongeza matumaini kwa wadau wengi wa muziki ambao kwa sasa wanatarajia kusikia mawe mapya na ya ukweli kutokana na mkali wao kusogea karibu na jiko zaidi.
Previous Post Next Post