MEMBE: M23 WAKITUCHOKOZA TUTAJIBU MAPIGO


membe 2d519
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianoa wa Kimataifa, Benard Membe

Dodoma. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Kimataifa Bernard Membe, amesema kuwa kamwe Tanzania  haitaogopa vitisho vinavyotolewa na Kikundi cha Waasi cha M23 cha DRC, huku akitoa masharti matatu kwa kikundi hicho kama hakitaki majeshi ya Tanzania yaende nchini humo.
Membe alisema hayo, akijibu hoja iliyotolewa na Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni kuwa kikundi hicho kimeandika barua ya wazi ikieleza kuwa, kisilaumiwe kama raia wa Tanzania watapatwa na mauaji ya halaiki ikiwa vikosi vya majeshi yake vitaenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

“Katika barua hiyo kiongozi huyo ametishia kwamba kikundi cha M23 kisilaumiwe kwa mauaji ya halaiki yatakayotokea kwa raia wa Tanzania endapo Serikali itaendelea na mpango wa kupeleka askari wake kujiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Congo DRC,” ilisema hotuba ya kambi ya upinzani.
“Katika barua hiyo kiongozi huyo ametishia kwamba kikundi cha M23 kisilaumiwe kwa mauaji ya halaiki yatakayotokea kwa raia wa Tanzania endapo Serikali itaendelea na mpango wa kupeleka askari wake kujiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Congo DRC,” ilisema hotuba ya kambi ya upinzani.
Akijibu hoja hiyo, Membe alikiri kuiona barua hiyo, aliyosema ilielekezwa kwake pamoja na Bunge na kusema kuwa lengo lake ni kutoa vitisho kutokana na kuogopeka kwa vikosi vya Tanzania.
“Kuhusu M23 nimepata barua wizarani na bungeni imeletwa, hiyo barua wanasema imeandikwa kwangu na Mungu na kuwa imesainiwa na Mungu, hawa wanatutisha kama  tulivyotishwa  na Kanali Mohamed Bakari alipokuwa ameiteka Anjwani, pamoja na vitisho vyote alivyotoa yeye ndiye aliyeishia kutoroka akiwa amevaa baibui,” alisema na kuongeza:
“M23 wanaua, wamebaka, wamedhalilisha wazee na mama, wameleta wimbi la wakimbizi zaidi ya 220,000, halafu wanamnukuu  Mwalimu Nyerere wakisema  binadamu wote ni sawa, huko ni kukufuru Kama  wangekuwa wanathamini kauli ya Mwalimu wasingeliua, wasingebaka, wasingedhalilisha  wazee.”
Alibainisha kuwa, waasi wa  kikundi hicho wamefanya uhalifu wa kutisha hadi kiongozi wao Bosco Ntaganda akaamua kujisalimisha kwenye vyombo vya usalama na kwa sasa amepelekwa katika  Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC.
“Kwa hiyo  M23  hawawezi kutufundisha ubinadamu, hawawezi kutufundisha amani na wala hawawezi kutumia jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kutuambia kitu kuwa binadamu wote ni sawa,” alisema.
Alisema kuwa, vikosi vitakavyokwenda DRC vitakuwa na kazi ya kutekeleza mambo matatu akitaja la kwanza kuwa ni  kuhakikisha M23 hawajipanui kutoka idadi ya 600 waliopo sasa,  kudhoofisha kundi hilo kwa kuondoa silaha mikononi mwao pamoja na kutengeneza uhusiano.
“Ni vizuri,  wale askari  tutakaowaona wapo bora waingie kwenye Jeshi la Taifa la DRC ili kuleta amani  pale na tutalinda amani pale. Wakituchokoza tutajibu mapigo, lakini lengo la kwenda pale siyo kupigana vita. Sisi tunaenda na mandate (mamlaka) ya Umoja wa Mataifa ‘chapter’ 7 ya Baraza la Usalama  la Umoja wa Mataifa,” alisema.
Aliongeza: “Jeshi letu ni imara sana, lenyewe halishindwi lipo Lebanon linafanya kazi nzuri na ya kusifiwa. Lipo Darfur la linafanya kazi nzuri ya kustahili kusifiwa; na Watanzania wajue kuwa ‘United Nation Mission ya Darfur’ sasa inaongozwa na jenerali Mtanzania  kuanzia mwezi  huu, kutokana na rekodi nzuri ya jeshi letu la Tanzania.
Ndiyo maana hao wanaobaka na kuua wakisikia tu Tanzania wanakwenda wanamsingizia Mungu, eti Mungu anawaunga mkono na Mwalimu Nyerere anawaunga mkono!”
“Wanataka  Bunge hili liseme Serikali isipeleke askari. Nalipongeza Bunge kwa uelewa mpana na kuungana kuwa kitu kimoja tunapokabiliana na vitisho vya aina hii.
Tanzania tuna nguvu, tuna historia, wakitaka M23 tusiende kule Alitaja mambo hayo kuwa ni; “Moja,  wafanye kama walivyofanya jana,(juzi) waanze kujitoa kwenye jeshi lile na kujisalimisha.
Pili,  yapo mazungumzo yanayofanywa na Rais Museveni Kampala ya kuitaka M23 pamoja na majeshi na Serikali ya DRC kukaa na kumaliza tofauti zao basi wamalize tofauti zao na kisha watupigie  simu kwamba wameshayamaliza  matatizo yote.”
Sharti la tatu ambalo Membe alitoa kwa kikundi hicho ni kutaka kikundi hicho kuacha mara moja vitendo vyao vya  kubaka, kuua na kuwafanya wananchi kuwa wakimbizi Kuhusu suala la Malawi, alisema:
“Mazungumzo yataanza rasmi kwa maana ya kuitwa kuhojiwa sisi akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mwishoni mwa mwezi huu ataenda Maputo, watakuwa wanahojiwa, ni imani  yetu Watanzania  kwamba jopo  la marais wastaafu linaloongozwa na  Joachim Chisano litafikia uamuzi.”
“Lakini ikishindikana  itabidi  tusonge mbele kwenda  ICJ, Tanzania hatutasita  kufanya hivyo na tuna kila aina ya ushahidi wa kuhakikisha kwamba tunashinda kesi hiyo,” alisema Membe. Chanzo: www.mwananchi.co.tz
Previous Post Next Post