MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA OAU/AU YAFANA



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akimkabidhi Mkuu wa Mabalozi na Balozi wa DRC hapa nchini, Mhe. Juma Khalfan Mpango Mwenge wa Umoja wa Afrika (OAU/AU) kuashiria kuanza kwa maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja huo yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam

"Brass Band" ikiongoza maandamano kutokea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuelekea Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 OAU/AU.

Mhe. Membe akishiriki maandamano hayo.

Mhe. Membe, Mabalozi, wananchi na wageni waalikwa wakiwa katika maandamano hayo kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika

Picha zaidi za maandamano.

Mhe. Membe akisikiliza Wimbo wa Taifa na AU zilizopigwa kuadhimisha miaka 50 ya umoja huo.

Picha zaidi wakati wa wimbo wa Taifa

Mhe. Membe, Mabalozi, na Viongozi wengine wakiangalia burudani kutoka vikundi mbalimbali vya utamaduni vilivyopamba maadhimisho hayo

Kikundi cha utamaduni kikitumbuiza.

Kikundi kingine cha burudani kilichopamba sherehe hizo.



Burudani ikiendelea.

Msemaji wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Umoja wa Afrika (AU) Bw. Emmanuel Luangisa ambaye ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoa hotuba wakati wa maadhimisho hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.



Mhe. Membe akitoa hotuba wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya AU-OAU. Wengine katika picha ni Mhe. Balozi Juma Khalfan Mpango (kulia), Mkuu wa Mabalozi, Mhe. Ambrosio Lukoki (kulia kwa Waziri), Mkuu wa Mabalozi wa Nchi za Afrika na Balozi wa Angola hapa nchini na Bw. John Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa





Mhe. Membe akiendelea na hotuba yake.



Mabalozi wa nchi mbalimbali waliopo hapa nchini wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)



Sehemu nyingine ya Mabalozi wakimsikiliza Mhe. Membe.



Mabalozi na wageni waalikwa wakimsikiliza Mhe. Membe.



Balozi Walidi Mangachi akiwasilisha mada kuhusu "Pan-Africanism and African Renaissance" wakati wa maadhimisho hayo huku Mhe. Membe, Mabalozi na Wageni waalikwa wakimsikiliza.



Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bi. Tonia Kandiero akiwasilisha mada kuhusu mchango wa benki hiyo katika maendeleo ya Afrika.



Wageni waalikwa wakisikiliza mada mbalimbali zilizowasilishwa.




Previous Post Next Post

Popular Items