Msanii wa nyimbo za injili ambaye pia ni mjasiriamali Bi. Elizabeth Benard akiimba wimbo wa "anafanya jambo" katika warsha ya wanawake wajasiriamali zaidi ya 150.Warsha hiyo iliandaliwa na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Dare to Dream,na kudhamaniwa naVodacom Tanzania,Benki ya CRDB na kinywaji cha Multa.Iliyofanyika jijini Dar es Salaam
.Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania walioshiriki katika warsha ya wanawake wajasiriamali wadogo na wa kati,iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Dare to Dream,na kudhamaniniwa naVodacom Tanzania,Benki ya CRDB na kinywaji cha Multa,Warsha hiyo inayofanyika mara moja kwa mwaka ilifanyika jijini Dar es Salaam kwa kuwashirikisha wanawake zaidi ya 150.
Mkufunzi na Mtaalamu wa maswala ya ujasiriamali Bi.Rehmah Kasule,akitoa elimu kwa wanawake zaidi ya 150 juu ya kuwawezesha kujua mbinu za kujiendeleza katika kukuza biashara zao,Warsha hiyo iliandaliwa na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Dare to Dream,na kudhamaniniwa naVodacom Tanzania,Benki ya CRDB na kinywaji cha Multa,na kufanyika mara moja kwa mwaka jijini Dar es Salaam.
WANAWAKE wajasiriamali wa Kitanzania wanayo nafasi nzuri ya kufanikiwa katika biashara zao ikiwa watajiamini na kuwa na uthubutu katika shughuli zao
Akizungumza wakati wa semina ya wanawake wajasiriamali iliyoambatana na maonyesho ya bidhaa mbalimbali jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Afisa mtendaji mkuu wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Dare to Dream foundation iliyoandaa semina hiyo Emelda Mwamanga alisema kutojiamini ni moja kati ya sababu zinazowafanya wanawake wajasiriamali kushindwa kusonga mbele
Emelda alisema kuwa, duniani ya sasa ya kibiashara imejaa ushindani mkubwa na bila kujiamini itakuwa ni vigumu kwa wanawake wajasiriamali kuweza kufanikiwa.
"Semina hii imewaleta pamoja wanawake wa kada mbalimbali ili kuweza kubadilishana uzoefu pamoja na kutiana moyo. Wapo waliofanikiwa kibiashara ambao watawaeleza wale ambao bado hawajafanikia njia walizopitia mpaka kufika hapo walipo. Kupitia semina hii watajifunza na namna ya kutengeneza bidhaa zenye viwango pamoja na namna ya kujitanga," alisema
Kwa upande wake Afisa masoko wa benki ya CRDB Emmanuel Kiondo alisema kuwa benki yake inatambua umuhimu wa kumwezesha mwanamke na ndiyo maana ikaamua kujitokeza kudhamini shughuli hiyo iliyolenga kuwajengea uwezo wanawake
Tunaamini kuwa mwanamke akiwezeshwa familia nzima inakuwa imewezeshwa. Benki ya CRDB imekuwa ikimjali sana mwanamke na tumeweza kuanzisha akaunti ya Malkia maalumu kwa ajili ya wanawake wenye malengo mbalimbali ikiwemo ya kiujasiriamali," alieleza
Mwakilishi kutoka kampuni ya Vodacom ambao ndiyo wadhamini wakuu wa semina na maonyesho hayo Alice Lewis alisema Vodacom inatambua mchango wa wanawake katika maendeleo ya jamii na itaendelea kuwa mstari wa mbele kuwasaidia kusonga mbele.