Ingawa wakili wa Lauryn Hill aliviambia vyombo vya habari kuwa mteja wake ameshalipa karibu $970,000 ya kodi aliyokuwa akidaiwa, jaji wa huko in Newark, NJ jana alimhukumu rapper huyo kifungo cha miezi mitatu jela.
Wakati wa kusikilizwa kesi hiyo, Lauryn alijitetea kuwa alipotea kwenye biashara ya muziki lakini alidhamiria kujiweka sawa.
“Niliwekwa kwenye system ambayo sikujua uhalisia wake. Mimi ni mtoto wa mtumwa wa zamani. Niliuza kopi milioni 50 na saa nipo hapa kulipa deni la kodi. Kama hiyo haifanani na utumwa basi sijui ni nini,” alisema mahakamani.
Pamoja na utetezi huo, jaji alitoa hukumu hiyo ya miezi mitatu jela, miezi mitatu chini ya ulinzi wa nyumbani na miezi 9 ya kuangaliwa akiwa nje.