KATIKA KUSHEHEREKEA BIRTHDAY YA BINTI YAKE SWIZZ BEATZ AWAPELEKIA PARIS MKEWE ALICIA KEYS NA EX GIRFRIEND WAKE JAHNA




Weekend iliyopita producer Swizz Beatz aliamua kuifurahisha familia yake kwa kusheherekea birthday ya binti yake jijini Paris, Ufaransa huku akiwa na watoto wake wote, mke wake wa sasa Alicia Keys na Jahna Sebastian ambaye ni mpenzi wake wa zamani na mama wa mwanae Nicole aliyekuwa anatimiza miaka 5.


Hit maker wa “Girl on fire” Alicia Keys ambaye ni mama wa mtoto wa kiume wa Beats aitwaye Egypt alionekana kuelewana vizuri na Jahna mama wa mtoto mwingine wa Beatz ambao waliungana pamoja na watoto wao katika hifadhi ya Disneyland huko Paris kwaajili ya kusheherekea birthday ya Nicole aliyekuwa anafikisha miaka 5.



Familia hiyo ilitokea London, Uingereza kwa private jet ambako Alicia Keys alikuwa ana perform weekend iliyopita.
Previous Post Next Post