Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akitangaza zawadi kwa Mshindi wa Kwanza wa Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar 2013/14,katika ukumbi wa Mikutano wa Kilimanjaro House,Masaki jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Ligi kuu ya Zanzibar,Consolata Adam.
Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam akizungumzia kuhusu maandalizi ya shamra shamra hizo za siku hiyo ya Jumamosi Mei 4,2013 katika uwanja wa Amani, Zanzibar..
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah akikabidhi Kombe atakalokabidhiwa Bingwa wa Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar,kwa Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam.