Filamu ya Without Daddy itakayomuonesha mama yake Kanumba kama muigizaji mkuu, inaingia sokoni wiki hii na huku mashabiki wa Kanumba wakitarajia kupata uthibitisho kuwa, kipaji cha uigizaji alichokuwa nacho kipo pia kwenye damu ya mama yake.
Filamu hiyo itakayosambazwa na kampuni ya Steps Entertainment imekuja mwaka mmoja tangu kifo cha Steven Kanumba.
Hiyo sio filamu ya kwanza iliyotoka kuelezea maisha baada ya kifo chake kwakuwa tayari zipo filamu zingine ikiwemo ya Jacky Wolper, After Death.