Chelsea
Torres akishangilia bao
Patrick Kluvert akiingia na kombe uwanjani
Torres akichezewa rafu
Baada ya kuvuliwa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani ulaya walioutwaa mwaka jana, kukosa ubingwa wa England na kombe la FA nchini Uingereza, hatimaye wazee wa London, klabu ya Chelsea wamefanikiwa kupunguza machungu baada ya kutwaa ubingwa wa ligi ya Uropa usiku wa kuamkia leo.
Chelsea wameifunga Benfica 2-1 katika mchezo wa fainali na shukuruni za pekee ni kwa beki wake Branislav Ivanovic aliyefunga bao dakika ya lala kwa buriani (Dakika 93) na kumpatia kocha wake wa muda Rafa Benitez atakayeondoka baada ya msimu huu na kumpisha kocha mwingine anayesemekana kuwa Jose Mourinho.
Hakika ubao wa matangazo wa dimba la Amsterdam mpaka dakika ya 90 ulikuwa unasomeka 1-1 na watu wengi wakaamini timu hizo zinaenda kutumia sheria nyingine ya mashindano.
Wakati watu wakijiandaa kupata dakika nyingine, Ivanovic alichafua hali ya hewa kwa Benfica na kuleta furaha kubwa sana kwa mashabiki wa Chelsea waliosafiri kutoka London mpaka Uholanzi kuwashangilia vijana wao.
Haikuwa kazi nyepesi kwa Chelsea kushinda mchezo wa jana usiku, lakini jinsi walivyoonekana kujituma muda wote walionesha kuwa na umoja mkubwa sana huku Kocha Benitez akiwahamasisha muda wake ili kubeba ndoo na kuondoka kwa amani. Channzo: sportmail