BILIONEA WA MAN CITY KUANZISHA TIMU MPYA MLS



1 35523
Sheikh Mansour (katikati) anataka kuwekeza MLS dola Milioni 100

MMILIKI wa Manchester City, Sheikh Mansour wa Abu Dhabi yupo karibuni kuwekeza kiasi cha dola za Kimarekani, Milioni 100 kuanzisha timu mpya itakayoshiriki katika Ligi Kuu ya Marekani, ijulikanayo kama Major League Soccer ambayo itakuwa na maskani New York.

Bilionea huyo wa waliokuwa mabingwa wa Ligi Kuu England, amekuwa katika mazungumzo mazito na ya siri na MLS kwa miezi kadhaa juu ya kuingiza timu mpya ya nguvu USA.
 
Sheikh ana matumaini yeye na Maofisa wa MLS, watakuwa kwenye nafasi ya kutangaza mpango huo wakati kikosi cha Roberto Mancini kitakapokwenda Marekani kucheza na Chelsea Jijini New York katika mchezo maalum wa hisani mwishoni mwa mwezi ujao.
 
 
 
Previous Post Next Post