AKUNA PRODUCER WA KUSHINDANA NA MIMI KWENYE KILL MUSIC AWARDS ASEMA "PANCHO"



Beatmaker wa B’Hits Music Group, Pancho Latino amesema hajaumia kutotajwa kwenye tuzo za Kili kwenye kipengele cha mtayarishaji bora wa muziki mwaka huu kwasababu hana producer wa kushindana naye.


Akiongea jana kwenye kipindi cha The Jump Off cha Times FM 100.5, Pancho amedai kuwa yeye hashindani kama maproducer wengi wanavyofanya.

“Sina competition, sababu kama ningekuwa nashindana na wale labda level yangu ingekuwa sawa na wale waliochaguliwa kwenye nominations. Mimi sishindani kwasababu mimi sipo level yao na sifanani nao,” alisema Pancho.

“Wangeniweka pale ingekuwa tatizo nakwambia,” alisisitiza.

The Jump Off huendehswa na Saleh Jabir. Msikilize zaidi hapa akimhoji Pancho na crew nzima ya B’Hits:


Previous Post Next Post