ZIARA YA KINANA YAMALIZIKA MOROGORO KWA KUTEMBELEA MRADI YA MAENDELEO


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Meneja Mradi wa mashamba ya Mfano ndani ya kijiji cha Pangawe,wilaya ya Morogoro vijijini,Bwa.Kim Sun Ho wa KOICA walipokuwa wakitembelea Shamba hilo lenye Wakaaazi wapatao 180,ambao wanasimamiwa na kupewa mafunzo ya Kilimo cha kisasa na ufugaji bora kutoka kwa shirika la Maendeleo la Korea (KOICA).


Kinana na Ujumbe wake wa chama hicho walitembelea mradi huo katika ziara yao ya kichama,Wakaazi hao wanamiliki zaidi ya hekari 150 kila mmoja ana magunia nane ya mahindi waliyovuna mwaka jana huku wakiwa na na kiasi cha shilingi milioni 50 benki.CCM imefanya ziara katika Wilaya ya Morogoro vijijini na kufungua mashina na matawi ya chama hicho huku akipokea wanachama wapya waliojiunga na waliotoka vyma vya upinzani.


Sehemu ya Shamba la mfano la Mahindi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa Meneja Mradi wa KOICA,Bwa.Kim Sun Ho wa KOICA,alipotembelea mradi wa majengo yatakayotumika katika mafunzo ya ufugaji wa kisasa katika kijiji cha Pangawe,Wilaya ya Morogoro Vijijini.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akijadili jambo na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM,Nape Nnauye walipotembelea mradi wa majengo yatakayotumika katika mafunzo ya ufugaji wa kisasa katika kijiji cha Pangawe,Wilaya ya Morogoro Vijijini.

Pichani ni Sehemu ya soko la Kisasa la Mkuyuni linalojengwa na CCM kwa gharama ya shilingi milioni 100,katika kata ya Mkuyuni,ndani ya Morogoro Vijijini.


Ndugu Kinana na ujumbe wake wa CCM wakielekea kukagua ujenzi unaoendelea wa kituo cha afya (zahanati) ya Mkuyuni.

Ujenzi wa jengo la kituo cha zahanati ya Mkuyuni ukiendelea .

Mmoja wa Wahudumu wa kituo cha afya cha Mtamba-Matombo wilaya ya Morogoro Vijijini, kilichopandishwa hadhi na kuwa Zahanati,Bi.Lilian Peter Haule akitoa maelezo mafupi ya maendeleo ya upanuzi wa ujenzi wa zahanati hiyo ya Mtamba kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurlhaman Kinana.
Previous Post Next Post