WASHIKA BUNDUKI WA LONDON WAIBUA MATUMAINI YA KUCHEZA LIGI YA MABINGWA, WAKUNG`UKA 3-1!





Urejeo wa kiungo bora wa Arsenal Jack Wilshere umewasaidia Arsenal kupata ushindi wa mabao 3-1 ya dakika za lala kwa buriani dhidi ya klabu ngumu ya Norwich City katika dimba la Fly Emirates na kuifanya klabu hiyo ipande nafasi ya nne na kuibua matumaini ya kucheza ligi ya mabingwa ulaya mwakani.
Wikiendi hii Chelsea na Tottenham hawachezi kwa sababu ya Nusu Fainali ya Kombe la FA, washika bunduki hao wa jijini London wanaweza kufanya vizuri na kucheza UEFA msimu ujao hivyo kuondoa machungu kwa mashabiki wake kwani hawana uwez0 wa kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka nchini Englanf msimu huu.

Katika mchezo huo, Norwich walianza kutikisa nyavu za Arsena kupitia kwa Michael Turner dakika ya 56, lakini kiungo hodari mwenye kiwango kizuri Emirates, Mikel Arteta akasawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 85, kabla ya Bassong kujifunga dakika ya 88 na kuipa Arsenal bao la pili, Mjerumani mwenye sifa ya kufumania nyavu Lukas Podolski alihitimisha kipute hicho baada ya kuandika bao la tatu na la ushindi dakika ya 90.
Katika mchezo huo, kikosi cha Arsenal kilikuwa; Fabianski, Sagna/Oxlade-Chamberlain dk80, Vermaelen, Koscielny, Gibbs, Arteta, Wilshere/Walcott dk59, Ramsey, Cazorla, Giroud na Gervinho/Podolski dk59.

Norwich: Bunn, Martin, Whittaker, Bassong, Turner, Johnson/Fox dk62, Snodgrass, Howson, Tettey/Jackson dk90, Holt na Kamara.
Matokeo mengine ya ligi kuu soka nchini England hapo jana ni yalikuwa kama ifuatavyo;

Reading 0-0 Liverpool
Southampton 1-1 Westham united
Everton 2-0 Queens Park Rangers
Aston Villa 0-0 Fullham







Kipa Mark Bunn akimkoromea mshika kibendera baada ya kuwapa Arsenal penalti

Lukas Podolski baada ya kuzamisha bao lake dakika ya 90 ambazo hazimruhusu kuku kumeza punje ya mchele 


Michael Turner akiifungia timu yake bao
Previous Post Next Post