TUICO MOROGORO WAFANYA MKUTANO WAO MKOANI MOROGORO


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya, akilakiwa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri, TUICO, katika ukumbi wa Midland Inn, Morogoro jana, muda mfupi kabla ya hafla ya kumtunuku cheti cha uanachama wa heshima ndani ya chama hicho, kama ishara ya kuenzi mchango wake.

Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Profesa Issa Shivji, kushoto, akilakiwa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri, TUICO, katika ukumbi wa Midland Inn, Morogoro jana, muda mfupi kabla ya hafla ya kumtunuku cheti cha uanachama wa heshima ndani ya chama hicho, kama ishara ya kuenzi mchango wake.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri, TUICO, Omary Ayub Juma wa kwanza kulia, akiimba wimbo wa mshikamano muda mfupi kabla ya kuanza hafla ya kuwatunuku vyeti vya heshima baadhi ya wanachama wake wastaafu kama ishara ya kuenzi mchango wao ndani ya chama, (katikati) ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Boniface Nkakatisi.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF, Crescentius Magori, akitoa mada mbele ya Wajumbe wa Baraza Kuu la TUICO, (hawapo pichani) Morogoro jana, pamoja na mambo mengine alisisitiza kuwa Mfuko huo tofauti na mifuko mingine hutoa mafao ya moja kwa moja kwa mwanachama husik bila kupitia kwa mwajiri wake, na kwamba Pensheni hutolewa kulingana na hali ya maisha kwa wakati huo.
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA