TIMU 14 KUSHIRIKI TAMASHA LA MEI MOSI



 Meneja mahusiano ya nje-Vodacom Tanzania,Salum Mwalimu akifafanua zaidi kuhusiana na udhamini wa kampuni hiyo kwenye tamasha la soka la kuadhimisha sikukuu ya Wafanyakazi nchini,ambapo timu kumi 14 zimepangwa kushiriki.Kulia ni Ofisa Udhamini na Matukio Bwa.Kaude Ibrahim,Mkuu wa Idara ya Michezo-Clouds Media Group Shaffih Dauda na mwisho kabisa kushoto ni Mwakilishi kutoka THT ambao pia watashiriki kutoa burudani kwa ujumla.

MKUU WA IDARA YA MICHEZO-CLOUDS MEDIA GROUP SHAFFIH DAUDA (PILI KULIA) AKIZUNGUMZA MBELE YA WANAHABARI (HAWAPO PICHANI) MAPEMA LEO KWENYE VIWANJA VYA LIDAZ CLUB KUHUSIANA NA KUFANYIKA KWA TAMASHA LA SOKA LA KUADHIMISHA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI NCHINI,AMBAPO TIMU KUMI 14 ZIMEPANGWA KUSHIRIKI. 
=========  ======== ======

TIMU 14 KUSHIRIKI TAMASHA LA MEI MOSI

Tamasha la soka la kuadhimisha sikukuu ya wafanyakazi nchini litafanyika siku ya jumatano (Mei Mosi) kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini.
Tamasha hilo lililoandaliwa na kampuni ya Butterfly Advertizing and Marketing kwa kushirikiana na Sports Extra and Sports Bar , litashirikisha jumla ya timu 14 za makampuni mbalimbali ya hapa jijini kwa mujibu wa mratibu wake, Shafii Dauda.
Dauda alizitaja kampuni hizo kuwa ni Benki ya CRDB, NMB, Vodacom Tanzania, Clouds Media group, Infinity Communications, Tanzania Cigarette Company (TCC),  NSSF, TBL, Tanesco, National Housing Corporation (NHC), Simbanet, Fastjet, Umoja Water na  DHL.
Alisema kuwa Vodacom Tanzania na NMB ndiyo wadhamini wakuu wa tamasha hilo lililopangwa kuanza saa 3.00 asubuhi na kupambwa na bendi ya Sky Light na Tanzania House of Talent (THT).
Kwa mujibu wa Dauda, timu hizo zitagawanywa katika makundi manne na kucheza kwa mchezo wa ligi na mshindi wa kwanza na wa pili wa bonanza hilo watazawadiwa vikombe na timu nyingine shiriki zitapewa vyeti.
Alisema kuwa sababu kubwa ya kuandaa bonanza hilo lililopangwa kumalizika saa 2.00 usiku ni kuwakusanya pamoja na kubadilishana mawazo wafanyakazi katika siku yao hiyo muhimu.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom, Salum Mwalimu  alisema kuwa sababu kubwa ya kudhamini na kushiriki katika bonanza hilo ni kuwapa zawadi wateja wao kwani wanaaminikuwa timu zote shiriki ni wateja wao.
“Mbali ya kudhamini, sisi tutashiriki na timu yetu, tunataka kuwaonyesha kuwa hata soka nasi tunacheza, tunawataka mashabiki kufika kwa wingi kwani ni hakuna kiingilio,” alisema Mwalimu.
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA