TANZANIA INA WATUMIAJI WA FACEBOOK ZAIDI YA LAKI 6 NA NUSU KILA MWEZI NA WENYE ACCOUNT AMBAZO NI ACTIVE!

Kwa mujibu wa mtandao unaohusika na utoaji takwimu za matumizi ya mitandao ya kijamii duniani, socialbakers, Tanzania ina watumiaji active (Monthly Active Users, MAU) 693,080 kila mwezi.



Idadi hiyo inaifanya Tanzania kuwa nchi ya 94 duniani kwa utumiaji wa mtandao huo wa kijamii. Takwimu hizo zinaonesha kuwa asilimia 71 ya watumiaji nchini ni wanaume na asilimia 29 ni wanawake.

Kundi kubwa la watumiaji wa Facebook Tanzania ni wale wenye umri kuanzia miaka 18-24 ambao idadi yao ni 295 020 wakifuatiwa na wale wenye umri kuanzia miaka 25-34.
Previous Post Next Post