SHEREHE ZA 49 ZA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZA FANA NEW YORK




Mh.Balozi Ramadhan Mwinyi ndiyo alikuwa mgeni mharikwa katika sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 49 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika jijini New York. Sherehe hiyo ilihudhiliwa na watanzania wengi kutoka katika miji ya jilani na New York kama New Jersey, Delaware, Massachusetts na Connecticut. Watanzania waliungana kwa pamoja kwa kula chakula na kucheza music sambamba na vinywaji baridi.
Katibu wa jumuiya ya watanzania New York bwana Shaban Mseba akisoma risala katika sherehe hizo za muungano
Mwenyekiti wa jumuiya Hajji Khamis akiongea machache mbele ya watanzania waliojitokaza katika sherehe hizo zilizofanyika New York katika kitongoji cha New Rochelle.
Dr Chemponda alikuwa nae kama anavyoonekana katika picha akiongea machache juu ya jinsi gani anavyo ujua muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mama Ashura Duale nae anaujua sana muungano wa Tanganyika na Zanzibar na alikuwa mmoja ya washuhuda wa uchanganyaji mchanga wa pande zote mbili za Tanganyika na Zanzibar
Hii ndiyo cake ya muungano ikiwa mezani
Ukodak wa pamoja katia ya Dr Chemponda, kushoto mama Ashura katikati, na kushoto kwa mama Ashura ni mama mwenye nyumba wa Mh. Balozi Mwinyi, Na kulia na Mh. Balozi Mwinyi
Ukodak mbele ya cake 
Mh. Balozi akikata Cake tayari kwa kuwalisha wana muungano walio jitokeza katika sherehe hizo
Mh. Balozi Ramadhani Mwinyi akimrisha kipande cha cake mama mwenye nyumba wake kabla ya watu wengine awajapata nafasi hiyo. Kwa picha zaidi ya sherehe hizo zilizofanyika katika jiji la New york
Previous Post Next Post