MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA WIKI YA CHANJO KITAIFA.

 Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, na  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia  mamia ya wananchi waliohudhuria kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo nchini iliyofanyika kitaifa huko Mlandizi , Mkoani Pwani tarehe 22.4.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpatia chanjo ya motto Haula Mlondwa ,miezi 6, kutoka katika kijiji cha Vigwaza, wilayani Kibaha, ikiwa ni uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo kitaifa iliyoadhimishwa huko Mlandizi tarehe 22.4.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akinamama na akina baba waliowaleta watoto wao kwa ajili ya chanjo wakati wa uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo kitaifa iliyofanyika huko Mlandizi, wilayani Kibaha tarehe 22.4.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahi na mtoto Haula Mlondwa, mwenye umri wa miezi  6 ambaye aliletwa kwenye sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa huko Mlandizi, katika wilaya ya Kibaha, na baba yake mzazi Bwana Mlondwa Omar , mkazi wa Vigwaza.  Mama Salma alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo tarehe 22.4.2013.  Bwana Mlondwa Omar alikuwa ni miongozi mwa wanaume wawili tu walioweza kuwaleta watoto wadogo kwenye chanjo wakiambatana na wake zao.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikweteakipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa maabara wa kituo cha afya cha Mlandizi ,wilayani Kibaha katika mkoa wa Pwani, Bwana Sostenes  Nyang’olo, jinsi ya kuchukua vipimo vya damu na makohozi kutoka kwa wagonjwa wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa iliyofanyika huko Mlandizi tarehe 22.4.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mheshimiwa Dr. Seif Rashid wakishiriki kuimba na kikundi cha kwaya cha Anglican Compassion kutoka Bagamoyo wakati wa uzinduzi rasmi wa chanjo kitaifa ulifanyika katika kijiji cha Mlandizi  tarehe 22.4.2013.


  Viongozi, wageni na wananchi  mbalimbali waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa kwa watoto wenye umri wa chini ya mwaka mmoja iliyofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Mtongani iliyoko Mlandizi katika wilaya ya Kibaha tarehe 22.4.2013.  
Previous Post Next Post

Popular Items