Dudu Baya kibiashara zaidi



Toka pande za Mwanza alipoweka maskani yake, msanii Godfrey Tumaini 'Dudu Baya' anasema kimya chake kwenye muziki kinatokana na biashara anazofanya ambazo hakuwa tayari kuzitaja.

Kwa mujibu wa Dudu Baya amekuwa akisafiri sana mikoani lakini Mwanza ndio kituo kikubwa cha biashara zake.

Dudubaya alikanusha taarifa ambazo ziliwahi kusambaa kwenye mitandao ya jamii kuwa bado anaendelea na tabia yake ya ugomvi na akiwa Mwanza aliwahi kumpiga mtangazaji wa kituo kimoja mkoani humo.

"Niko kwenye muziki toka mwaka 1997, sijawahi kumpiga mtangazaji yeyote.Kuna hata baadhi ya waandishi wa habari walikuwa wanaandika skendo ambazo hazikuwa za kweli lakini sikuwahi mpiga yeyote wakati wengine nawajua.Nawaheshimu sana watangazaji, MaDj na waandishi wa habari, mimi siku hizi sio mgomvi tena kama zamani", alieleza Dudubaya.
Previous Post Next Post