Sir Alex Fergusson amesema hatompumzisha mshambuliaji wake Robin Van Persie kwenye mechi ya jumatatu dhidi ya Manchester City kwa sababu anafahamu ni kawaida kwa washambuliaji kupitia kipindi cha ukame wa mabao kama anachopitia Van Persie kwa sasa ndio maana hadhani kama kumpa Mshambuliaji wake mapumziko ndio suluhisho la ufungaji.
Robin Van Persie hajafunga goli lolote kwa michezo tisa sasa ikiwa ni kipindi chake kirefu bila kufunga tangu alipokwenda England akitokea Uholanzi ambapo jumamosi alidhani amefunga kwenye mechi dhidi ya Sunderland lakini kamati maalum ya ligi kuu ya England iliamua kuwa goli hilo lilikuwa la kujifunga la Titus Bramble hali inayofanya kipindi cha RVP bila kufunga goli lolote kuwa kirefu zaidi.
United inacheza na Manchester City jumatatu huku ikiongoza msimamo wa ligi kuu ya England kwa tofauti ya pointi 15 ambapo ushindi dhidi ya mabingwa hao watetezi utafanya tofauti hiyo kuongezeka hadi kufikia pointi 18 huku Sir Alex Fergusson akithibitisha kurejea kwa wachezaji Wayne Rooney na Rafael Da Silva ambao walikuwa majeruhi, pia anatarajia kurejea kwa wachezaji wengine wawili ambao ni Johny Evans na Nemanja Vidic.